Obama azionya nchi zisitegemee Marekani

Rais Barack Obama akizungumza kando mwa mkutano wa viongozi wa jumuiya ya APEC, ameonya kuwa nchi yoyote isitegemee kuwa inaweza kutajirika kwa kusafirisha bidhaa Marekani.

Image caption Barack Obama

Bw Obama alisema mataifa yenye uzalishaji mkubwa katika kile kinachoonekana wenye uchumi mkubwa barani Asia, kama vile China na Japan yanapaswa kuachana na hali yenye utata kutegemea usafirishaji bidhaa na badala yake yachukue hatua ya kuimarisha masoko ya ndani.

Matamshi yake ameyatoa wakati viongozi wa mataifa 21 ya eneo la Pacific (APEC) wakikutana mjini Yokohama nchini Japan.

Viongozi hao watajadili mpango wa kubuni eneo huru la kibiashara.