Kuna hofu ya kuzuka vita vipya Sudan-UN

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Image caption Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na madai ya ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Sudan Kaskazini na Kusini.

Amesema hali hiyo huenda ikasababisha mzozo mkubwa zaidi na hivyo kuhujumu kura ya maoni kuhusu uhuru wa Sudan Kusini iliyopangiwa kuandaliwa mwezi januari hapo mwakani.

Pande zote mbili zimesema kuwa zitaheshimu matokeo ya kura hiyo ya maoni.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, William Hague, naye ameonya kuwepo na matumaini makubwa kuhusu ufanisi wa kura ya maoni ya Januari 9.

Zoezi la kuandikisha raia wa Sudan Kusini, kabla ya kura hiyo ya maoni, ilianza Jumatatu iliyopita.