Acheni kutoa picha zisizofaa za Rais-Uganda

Rais wa Uganda
Image caption Rais wa Uganda

Mkuu wa idara ya habari ya rais wa uganda Yoweri Museveni amesema kuwa sifa ya rais huyo imeharibiwa vibaya kutokana na mziki wa Rap aliouimba mwezi uliopita.

Tamale Mirundi amesema walaghai wameharibu picha za bwana Museveni, wakitumia komputa, na kumfananisha na nyota wa miziki ya Hip Hop anayeimba akiwa nusu uchi.

Baadhi ya picha hizo zinaonyesha amevalia mkufu shingoni huku akiwa na picha alizochorwa mwilini maarufu kama ''tattoos''.

Rais Museveni anawania muhula mwingine kama rais wa Uganda kutipia chama cha National Resistance Movement NRM.