Hali ya hatari yatagazwa nchini Guinea

Raia wa Guinea
Image caption Raia wa Guinea

Hali ya hatari imetangazwa nchini Guinea baada ya makabiliano makali kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa mgombezi wa kiti cha urais, Cellou Dalein Diallo, aliyeshindwa katika uchaguzi wa hivi maajuzi.

Watu wasiopungua wanane waliuwawa katika machafuko ya baada ya uchaguzi huo katika mji mkuu wa Conakry.

Katika tangazo lililotolewa kwenye televisheni ya kitaifa, mkuu wa majeshi Jenerali, Nouhou Thiam, amesema hali hiyo ya hatari itadumishwa hadi pale mahakama kuu itakapoamua matokeo kamili ya uchaguzi huo.

Mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi huo, Alpha Conde, amesema anataka kuongoza maridhiano ya kitaifa.

Marekani imeshutumu vikali machafuko hayo.

Wachunguzi wanahofia kwamba uhasama wa kikabila unaozidi kukua nchini kati ya wapinzani wa uchaguzi huo huenda ukaenea hadi mataifa jirani, hususan taifa la Sierra Leone.