Mashirika ya misaada yashutumiana Haiti

Shirika la msaada la madaktari wasio na mipaka la Medicins Sans Frontieres, limeshutumu jinsi mashirika mbali mbali yanavyokabiliana na maradhi ya kipindupindu nchini Haiti, ambapo hadi kufikia sasa watu elfu moja na mia mbili wamekwishakufa.

Image caption Kipindupindu Haiti

Kwenye taarifa yake shirika hilo limesema mahitaji ya wakaazi wa Haiti hayashughulikiwi ipasavyo licha ya idadi kubwa ya mashirika ya kutoa msaada kuwepo nchini humo.

Shirika la MSF sasa linataka hatua kuchukuliwa haraka na kujengwe vyoo, pamoja na kutolewa maji safi kwa wakaazi. Pia shirika hilo linataka watu wa Haiti wahakikishiwe maradhi hayo ambayo hayafahamiki vizuri nchini humo, yana tiba.

Kiongozi wa shirika la Umoja wa Mataifa nchini Haiti Edmund Mulet, alishutumu kile alichokitaja kitendo cha kihuni kiliochosababisha ghasia kuzuka nchini humo.