Tuzo ya Nobel kutokabidhiwa mtu

Kiongozi anayesimamia kamati inayotoa tuzo ya amani ya Nobel Thorjon Jagland, amethibitisha hakuna mtu yeyote atakayekabidhiwa tuzo hiyo la mwaka huu kwa niaba ya mshindi Liu Xiaobo ambaye yuko gerezani.

Image caption Liu Xiaobo

Bw Xiaobo ni mtetezi wa haki za binadamu nchini China. Jagland aliiambia BBC kuwa tuzo hily itahifadhiwa hadi pale bw Xiaobo aweze kuichukua mwenyewe. Ndio mara ya kwanza tangu 1936 tuzo hiyo kutochukuliwa na mshindi au jamaa wa karibu wa aliyetunukiwa.

Mkewe bw Liu anatumikia kifungo cha nyumbani.

Bwana Jagland vile vile alithibitisha kuwa China imewatumia barua mabalozi wake walioko Oslo ikiwaonya wasihudhurie hafla ya kutolewa tuzo hiyo.