Mali wafuzu chini ya miaka 17 mwaka 2011

Mali imejihakikishia nafasi ya kucheza mashindano ya Ubingwa wa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 mwaka 2011 baada ya kuwalaza Cameroon mabao 3-0 mjini Bamako.

Image caption Mali yafuzu chini ya miaka 17 Afrika

Mali wamefuzu kwa jumla ya mabao 4-0, baada ya ushindi walioupata ugenini wa bao 1-0 walipocheza mjini Yaounde.

Mali inaungana na wenyeji Rwanda pamoja na Misri, zikiwa ni timu pekee zilizojihakikishia nafasi kwa mashindano yatakayofanyika mwezi wa Januari.

Rwanda imefuzu kwa kuwa wenyeji, wakati Misri wamepata nafasi hiyo baada ya wapinzani wao Mauritius kujitoa.

Mabingwa watetezi Gambia inawabidi kujipapatua na kufuta deni la mabao 3-2 waliyofungwa na Tunisia ili kujihakikishia nafasi ya kutetea taji lao mwakani.