Israel isipoacha ujenzi mazungumzo kamwe

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas, amesema haitowezekana kurudi katika mazungumzo ya amani na Israel, ikiwa Israel haitaacha kuendeleza ujenzi wa makaazi katika maeneo yote wanayoyakalia, pamoja na Jerusalem Mashariki.

Image caption Mahmoud Abbas

Bwana Abbas alikuwa akijibu taarifa kwamba serikali ya Marekani imeiahidi Israel vivutio vya kijeshi na kidiplomasia, ili iache ujenzi wa makaazi katika Ufukwe wa Magharibi.

Bwana Abbas alisema, bado hajapata mwaliko rasmi kutoka Marekani wa kurudi tena kwenye meza ya mazungumzo, lakini alisema, hatorudi tena kwenye mazungumzo, iwapo ujenzi wa makaazi hautasitishwa kikamilifu.