Siku ya maombolezo ya kitaifa Cambodia

Image caption Polisi wakiwasaidia waathiriwa

Waziri mkuu wa Cambodia, Hun Sen ametangaza siku ya maombolezo ya kitaifa siku ya alhamisi kufuatia vifo vya takriban watu mia tatu hamsini katika mkanyagano uliotokea wakati wa sherehe za mwaka mpya za kumwagiana maji katika mji mkuu, Phnom Penh.

Tangazo hilo limetolewa na Waziri mkuu wakati maafisa wakiendelea kutambua miili ya waathiriwa wa mkasa huo uliowaacha mamia zaidi wakiwa wamejeruhiwa.

Image caption Mwanamke akiomboleza kifo cha jamaa yake Cambodia

Bwana Hun Sen aliahidi kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo- ambalo amelitataja kuwa mkasa mbaya zaidi kuwahi kutokea Cambodia tangu enzi ya Khmer Rouge katika miaka ya sabini.

Ameongeza kuwa serikali itawalipa jamaa za waliokufa dola alfu moja mia mbili hamsini kugharamia maziko ya wapendwa wao.