Jamie Carragher wa Liverpool aumia bega

Mlinzi imara wa Liverpool Jamie Carragher huenda akakosa kucheza soka kwa muda wa mwezi mmoja baada ya bega lake kuchomoka.

Image caption Jamie Carragher

Carraghe ambaye ni nahodha msaidizi wa Liverpool, aliumia katika mchezo wa ligi kuu ya England siku ya Jumapili, walipofungwa mabao 2-1 na Tottenham katika uwanja wa White Hart Lane.

Meneja wa Liverpool Roy Hodgson akielezea kuumia huko kwa Carragher baada ya mechi, alisema "Ni mbaya sana." "Ni jambo la kukatisha tamaa kumtokea mlinzi huyo akiwa anacheza mechi yake ya 450 ya Ligi Kuu ya England.

Ameongeza:"Kwa sasa hatutakuwa nae pamoja na Steven Gerrard na hao ndio nguzo ya klabu yetu."