Federer amshinda Nadal fainali ya ATP

Roger Federer ameelezea kumfunga Rafael Nadal na kumaliza ukame wa kukosa vikombe kwa miaka mitano, ni jambo muhimu na kueleza kushinda mjini London ni kitu maalum zaidi.

Image caption Roger Federer

Mcheza tennis hiyo raia wa Switzerland, alimfunga anayeshikilia nafasi ya kwanza ya ubora wa wachezaji wa tennis duniani, Nadal kwa seti 6-3 3-6 6-1 katika uwanja wa O2 Arena na kufanikiwa kushinda fainali za ATP World Tour, taji ambalo aliwahi kushinda mara ya mwisho mjini Shanghai miaka mitatu iliyopita.

Federer alisema:"Ni jambo zuri ajabu, nimefurahishwa sana na jinsi nilivyocheza wiki yote hii," "Kushinda mara ya tano hakina ni jambo la kujivunia, kwa mara ya tatu katika sehemu mbalimbali. Kama nilivyosema awali, ni jambo zuri sana kushinda mjini Houston, Shanghai na sasa hapa London.

Federer alitawala seti ya kwanza na ya tatu katika fainali hiyo iliyochezwa siku ya Jumapili kwa muda wa dakika 97 na alionekana yupo imara sana baada ya kufanikiwa kwenda sare bila ya kupoteza seti hata moja.

Alianza mwaka huu kwa ushindi, alishinda mashindano ya Australian Open, lakini akashindwa kusonga mbele katika fainali ya Grand Slam, hali iliyomfanya kupoteza rekodi yake ya kucheza nusu fainali kubwa mara 23 katika mashindano ya French Open kabla ya kupoteza mchezo hatua ya robo fainali dhidi ya Tomas Berdych huko Wimbledon.