Ndege ya mizigo yaanguka Pakistan

Takriban watu wanane walifariki dunia nchini Pakistan baada ya ndege ya mizigo kuanguka na kuwaka moto punde baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Karachi.

Image caption Ndege ya mizigo yaanguka Karachi Pakistan

Waliopoteza maisha yao walikuwa ni wafanyakazi wa ndege iliyotengenzwa nchini Urusi, ambayo ilikuwa inaelekea Sudan baada ya kuanguka kwenye eneo la makaazi ya watu karibu na uwanja wa ndege.

Mafuta ya ndege yalisababisha majengo kadhaa kuwaka moto.

Inadhaniwa kuwa mbali na wafanyakazi hao wa ndege, huenda watu wengine kadhaa waliokuwa kwenye eneo la ajali nao wamepoteza maisha yao.

Mwandishi wa BBC mjini Karachi, amesema endapo ndege hiyo ingeanguka kama mita 500, basi ingeathiri eneo kubwa lenye watu wengi.