Liverpool yasonga mbele

Liverpool imejihakikishia nafasi ya kucheza raundi ya timu 32 katika michuano ya Kombe la Europa, licha ya kipa Pepe reina kufanya makosa yaliyosababisha sare na Steaua Bucharest.

Image caption Roy Hodgson

Milan Jivanovic aliandika bao la kuongoza la Liverpool baada ya kugonga kichwa kutoka katika krosi ya Ryan Babel.

Lakini Reina aliachia kichwa cha Eder Bomfim kumpita katikati ya miguu yake, na kuwa bao la kusawazisha la Steaua Bucharest.

Kicha kingine kilichopigwa na Kyrgiakos kiligonga mwamba kabla ya mpira kumalizika na hivyo Liverpool kusonga mbele licha ya kupata hiyo pointi moja.

Haukuwa mchezo wa kuvutia sana kwa Liverpool, kwani timu yenyewe ilikuwa dhaifu.

wachezaji wanane wakuu wa Liverpool hawakucheza kutokana na kuwa majeruhi au kupumzishwa. Meneja Roy Hodgson amekuwa akibadili kikosi chake hasa katika michuano hii, ili kukuza vipaji vya wachezaji vijana, na pia kuwapa nafasi wachezaji wakongwe waweze kuonesha uwezo wao.