Newcastle yamtimua meneja wao Hughton

Klabu ya Newcastle United Football imetangaza kuachana na meneja wake Chris Hughton. Pia kocha wa walinda mlango Paul Barron naye anaondoka katika klabu hiyo.

Image caption Chris Hughton

Bodi ya klabu hiyo imesema inamshukuru Chris kutokana na jitahada zake wakati wa kipindi cha mpito kutoka ligi ya Championship na kurejea katika Ligi Kuu ya England.

Chris ameonesha kujituma kwa hali ya juu tangu alipoteuliwa kuwa meneja wa klabu hiyo mwezi wa Oktoba mwaka 2009. Klabu ya Newcastle imemtakia kila la kheria.

Bodi ya klabi hiyo kwa sasa inamtafuta meneja mwenye uzoefu wa hali ya juu ili kuiongoza vyama klabu hiyo.

Jukumu la kumtafuta meneja mpya limeanza. Tangazo litatolewa muda mfupi ujao wakati huu mipango ya uhamisho ikikamilika.