Tsvangirai apinga uchaguzi wa mapema

Image caption Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai. Bwana Tsivangirai anapinga pendekezo la kuandaa uchaguzi mkuu kabla ya kura ya maoni.

Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amesema kuwa uchaguzi wa mapema hauwezi kufanyika nchini humo bila mageuzi muhimu ikiwa ni pamoja na marekebisho ya katiba.

Bwana Changirai ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba Zimbabwe huenda ikakumbwa tena na machafuko kama yale ya mwaka 2008 iwapo uchaguzi utaandaliwa kabla ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya.

Mpinzani wa kisiasa wa bwana Tsangirai, rais Robert Mugabe---ambaye wanagawana naye madaraka---anasema anazingatia kuitisha uchaguzi mkuu mwezi juni hapo mwakani.