Wajumbe wa Zanu PF wakutana.

Image caption Rais Robert Mugabe

Nchini Zimbabwe, wafuasi wa chama cha rais Robert Mugabe Zanu-PF wanakusanyika mjini Lusaka kwa kongamano la kila mwaka la chama hicho.

Bwana Mugabe aliitisha uchaguzi wa mapema mwaka ujao wakati mkataba wa kugawana madaraka utakapokamilika na wajumbe katika mkutano huo wanatarajiwa kumwidhinisha bwana Mugambe kugombea kiti cha urais.

Lakini waandishi wanasema kuna mgawanyiko ndani ya chama hicho kuhusu ikiwa Zimbabwe inafaa kufanya uchaguzi wa mapema kabla ya mageuzi muhimu kutekelezwa.

Baadhi watu wanaamini kuwa uchaguzi wa mapema huenda ukasababisha Zimbabwe kutengwa zaidi na jamii ya kimataifa--na hivyo kuhujumu maendeleo ya kiuchumi ambaye yamepatikana hivi karibuni.