Kura ya Abyei Sudan kucheleweshwa.

Image caption Ramani ya jimbo la Abyei nchini Sudan. Marekani yasema kura ya kuamua mustakabal wa jimbo hili haitafanyika mwezi ujao.

Msemaji wa serikali ya Marekani, Philip Crowley, amesema kuwa kura ya maamuzi kuamua mustakabal wa eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Abyei nchini Sudan haitafanyika tarehe tisa mwezi Januari.

Bwana Crowley hata hivyo amesema kwamba serikali ya marekani itaendelea kuzitia hamasa pande zote husika kutafuta suluhu kuhusu hatma ya jimbo la Abyei.

Image caption Jimbo la Abyei

Kura hiyo ilikuwa imepangiwa kufanyika ili kuamua iwapo Abyei itaendelea kuwa sehemu ya Sudan Kaskazini ama itajiunga na Kusini.

Maafisa wa serikali ya Sudan mjini Khartoum tayari walikuwa wamelalamika kwamba hapatakuwa na muda wa kutosha kuandaa kura hiyo.

Leo jumatano ndiyo siku ya mwisho ya kuwaandikisha wapiga kura.

Kura nyingine ya maoni kuamua iwapo Sudan Kusini itajitangazia uhuru inatarajiwa kufanyika tarehe tisa mwezi Januari hapo mwakani.