Iran: Ondoeni vikwazo tuzungumzie nuklia

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amesema mazungumzo kuhusiana na mpango wa nchi yake kukuza nguvu za kinuklia, yatazaa matunda iwapo vikwazo ilivyowekewa nchi yake vitaondolewa.

Image caption Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad

Wapatanishi kutoka Iran pamoja na viongozi wa mataifa yenye ushawishi mkubwa, yaliendelea na mashauriano siku ya Jumanne mjini Geneva, huku mjumbe mkuu wa Muungano wa Ulaya, Catherine Ashton akisema wanapiga hatua.

Viongozi hao wamekubali kukutana tena mwisho wa mwezi wa Januari mwakani mjini Istanbul.

Siku ya Jumatatu, wapatanishi walitumia karibu saa kumi kwa mashauriano.

Wajumbe wa kudumu kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani, wanataka Iran kutii uamuzi wamaamuzi wa Umoja huo kuhusiana na mpango wake wa nuklia.

Mataifa ya Magharibi yanashuku Iran inataka kutengeneza silaha ikitumia nguvu za kinuklia jambo ambalo Iran inapinga.