Chanjo mpya homa ya mapafu yazinduliwa

Chanjo mpya ya kuzuwia homa ya mapafu ya pneumonia, imezinduliwa kwenye sherehe inayofanywa Nicaragua.

Image caption Bakteria wa homa ya mapafu

Chanjo hiyo itakuwa rahisi kushinda inavouzwa katika nchi tajiri, kwa sababu itagharimiwa na mataifa kadha, pamoja na Uingereza.

Mwakani, chanjo hiyo itaanza kutumiwa katika nchi nyingine 40 pamoja na Honduras, Kenya na Sierra Leone.

Chanjo hiyo itatoa kinga dhidi ya ugonjwa unaosababisha homa ya uti wa mgongo ama meningitis, na pneumonia, magonjwa yanayouwa watoto wengi sana walio

chini ya umri wa miaka mitano.