Wanajeshi wa serikali washambulia SLA

Vikosi vya kulinda amani nchini Sudan vimesema wanajeshi wa serikali wamefanya mashambulio ya siku mbili dhidi ya kundi moja la waasi katika jimbo la Darfur la Sudan Liberation Army.

Image caption Wanajeshi wa kulinda amani Darfur

Mtu mmoja aliuwawa na wengine kumi na sita kujeruhiwa katika haratati hizo zao kijeshi, katika kijiji cha (Khor Abeche) kilichopo Darfur Kusini.

Nyumba kadhaa zilichomwa moto na taarifa zinasema zaidi ya wanavijiji mia mbili wamekimbia nyumba zao.

Mapema mwezi huu, serikali ililishtumu kundi la Sudan Liberation Army kwa kukiuka mkataba wa amani uliotiwa saini miaka minne iliyopita.