Sri Lanka yabadili msimamo

Serikali ya Sri Lanka imebadilisha msimamo wake wa awali, na imetangaza sasa itaruhusu ujumbe wa haki za kibinaadamu, ulioteuliwa na Katibu Mkuu, kuzuru nchi hiyo.

Image caption Sri Lanka

Awali serikali ilipinga uteuzi wa ujumbe huo wa watu watatu, ambao utachunguza maswala ya ukatili uliofanywa wakati wa vita nchi humo.

Lakini waziri mmoja wa serikali, anashikilia msimamo kuwa ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, usiruhusiwe nchini.