Chelsea yalazimisha sare na Spurs

Didier Drogba ameshindwa kufunga mkwaju wa penati na kuipatia ushindi Chelsea, baada ya golikipa wa Spurs kupangua shuti lake.

Spurs waliandika bao lao kwa kwanza katika dakika ya 15 katika kipindi cha kwanza kupitia Roman Pavlyuchenko.

Didier Drogba ambaye alianza akiwa bench, aliingia katika kipindi cha pili na katika dakika ya 70, alimponyoka beki Michael Dawson na kuachia shuti ambalo Gomes alishindwa kuucheza.

Katika dakika za nyongeza, Gomes alimchezea rafu Ramires, na mwamuzi Mike Dean kupuliza kipenga cha penati. Didier Drogba alipiga mkwaju huo amabo Gomes aliupangua.

Kwa matokeo hayo, Chelsea sasa ina poini sawa na Manchester United 31, huku Arsenal na Manchester City zikiongoza zikiwa na pointi 32.