Dosari matokeo uchaguzi wa Belarus

Waangalizi kutoka Shirika la usalama la jumuiya ya Ulaya wamesema uchaguzi wa Urais uliofanyika Jumapili Belarus ulikumbwa na dosari kubwa.

Image caption Mfuasi wa upinzani akizungumza na askari wa Belarus

Rais Alexander Lukashenko aliibuka mshindi kwa kura nyingi zaidi baada ya uchaguzi huo.

Waangalizi kutoka Ulaya Magharibi na Mashariki wameliponda zoezi la kuhesabiwa kwa kura na kushutumu polisi waliotumia nguvu kupindukia kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana mjini Minsk baada ya matokeo kutangazwa.

Marekani na Umoja wa Ulaya wamelaani vikali uvamizi wa polisi uliyosababisha waandamanaji na wapinzani kupigwa na kuwekwa kizuizini.