Arsenal yainyuka Chelsea 3-1

Arsenal imejikita katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya England baada ya kuizaba Chelsea 3-1.

Image caption Fabregas aliandika bao la pili

Mabao kutoka kwa Alexander Song, Nahodha Cesc Fabregas na Theo Walcott ndio yalizamisha meli ya mabingwa hao watetezi.

Bao pekee la kufutia machozi kwa Chelsea lilifungwa na Branislav Ivanovic.

Arsenal sasa wamefikisha pointi 35, katika nafasi ya pili, huku Chelsea wakiendelea kusalia katika nafasi ya nne wakiwa wa pointi 31.