Mancini ataka ushindi wa nyumbani

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini, amewachagiza wachezaji wake kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo ya nyumbani.

Image caption Roberto Mancini

City ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Newcastle siku ya Jumapili katika sikukuu ya Boxing Day na wamekuwa na rekodi nzuri ya kushinda nje ya uwanja wa nyumbani katika michezo ya ya Ligi Kuu ya England, lakini wameshinda mechi nne tu katika ya tisa walizocheza nyumbani.

"Nafahamu hatuna budi kufanya vizuri kwa mechi nyumbani, na hili ni muhimu," alisema Mancini, ambaye kikosi chake kinajiandaa kupambana na Aston Villa siku ya Jumanne.

City walipoteza mchezo wake wa nyumbani tarehe 20 Desemba, walipofungwa mabao 2-1 na Everton.

Manchester City wangekalia kiti cha uongozi wa ligi kuu ya England, wakati wa sikukuu ya Krismasi, kama wangeshinda mchezo dhidi ya Everton.

"Msimu ni mrefu sana na tunahitaji kujipanga upya. Hatuna budi kuendelea na ushindi."

City pia ilipoteza mchezo wa nyumbani dhidi ya Arsenal na wakapoteza pointi walipocheza na Blackburn, Manchester United na Birmingham.