Watu themanini wauawa Nigeria kwa mabomu

Maafisa wa serikali ya Nigeria wamesema takriban watu themanini wameuwawa katika mfululizo wa mashambulio ya mabomu katikati ya nchi hiyo.

Image caption Machafuko katikati ya Nigeria

Shirika la kushughulikia mambo ya dharura nchini Nigeria limesema idadi hiyo ni kwa mujibu wa hospitali za eneo hilo.

Shirika hilo limesema takriban watu mia moja tisini wamejeruhiwa.

Machafuko hayo yalianza mkesha wa siku kuu ya Krismasi baada ya kutokea mashambulio ya mabomu katika mji wa Jos, ambao umekumbwa na machafuko ya kikabila na kidini katika siku za hivi karibuni.

Ghasia baadae zilifuatia kati ya vijana wa Kikristo na Kiislamu.