Khodorkovsky hatiani kwa ubadhirifu

Jaji mmoja nchini Urusi amemtia hatiani tajiri Mikhail Khodorkovsky, katika mashtaka ya pili ya ubadhirifu wa pesa yaliyokuwa yakimkabili.

Image caption Mikhail Khodorkovsky

Bw Khodorkovsky ambaye alikuwa mtu tajiri zaidi nchini Urusi, anaendelea kutumikia kifungo cha miaka minane gerezani kwa kosa la kukwepa kulipa ushuru.

Mashtaka ya pili ambayo amepatikana na hatia yalihusiana na ubadhirifu wa pesa za umma kupitia kampuni yake ya mafuta ya Yukos.

Wafuasi wake wamesema kesi inayomkabili imechochewa kisiasa.

Wakati wa utawala wa Rais Vladmir Putin, bw Khodorkovsky alikuwa akitoa ufadhili kwa vyama vya upinzani na kuishutumu serikali ya Urusi kwa kujihusisha na ufisadi.