Abou Diaby aumia tena

Kiungo wa Arsenal Abou Diaby huenda asiendelee kucheza soka kwa muda mwingine mrefu, baada ya kutengua msuli wa mguu, ikiwa ni muda mfupi baada ya kupona jeraha lake la awali la kiwiko cha mguu.

Image caption Arsenal yapata pigo la mchezaji

Mfaransa huyo, aliingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Chelsea walioshinda 3-1, baada ya kutocheza kwa wiki tisa.

Hata hivyo alitoka akichechemea katika sare ya 2-2 dhidi ya Wigan.

"Ni kutenguka kwa msuli," amesema meneja Arsene Wenger, akizungtumza na wavuti wa Arsenal. "Hatocheza kwa muda kidogo, wiki kadhaa nadhani."

Image caption Abou Diaby

Diaby alivunjika mguu, na kutengua kiwiko mwaka 2006, kabla ya kurejea tena uwanjani.

Tatizo la kuendelea kuumia kwa mchezaji huyo wa Ufaransa kutaleta wasiwasi katika kikosi cha Arsenal ambacho kinapigana na vigogo wengine katika nafasi za juu katika msimamo wa ligi kuu ya England.

Manchester United iko kileleni, ikiwa pointi sawa na mahasimu wao wa mji mmoja, Manchester City, tofauti ikiwa ni magoli huku zote zikiwa na pointi 38.

Image caption Diaby

Sare dhidi ya Wigan iliipokonya safasi Arsenal ya kuwa na pointi sawa na timu hizo za Manchester, na hivy kusalia katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36.

Tatizo la mwanzo kwa Diaby lilianza mwezi Septemba baada ya kufanyiwa rafu na mlinzi wa Bolton Paul Robinson.

Kiungo huyo wa Arsenal alikaa nje kwa wiki tisa kutokana na jeraha la kiwiko cha mguu baada ya kucheza dhidi ya Birmingham Oktoba 6, ambapo Arsenal ilishinda 2-1.

Diaby ameichezea Arsenal mara tisa tu msimu huu katika mechi za ligi kuu, na kufunga bao moja tu.

Diaby alitokea Auxerre ya Ufaransa mwaka 2006 kwenda Arsenal kwa thamani ya Pauni milioni 2.