Somaliland yawahukumu Warusi sita

Hargeisa, Somaliland
Image caption Hargeisa, Somaliland

Mahakama moja ya serikali ya Somaliland imewahukumu kifungo gerezani Warusi sita waliokuwa wafanyikazi wa ndege iliyotekwa nyara mapema mwezi huu ikiwa ikisafirisha silaha za kivita.

Inasemekana silaha hizo zilikuwa zikilpelekwa katika eneo la Puntland linaloendesha shughuli zake huru nchini Somalia.

Watuhumiwa walihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kutozwa faini ya dola mia tano kila mmoja wao kwa kusafirisha silaha kwa eneo ambalo linakisiwa kuwa adui wa Somali na kwa ukiukaji wa sheria za anga za eneo la Puntland.

Sare za wanajeshi na vilipusi vilinaswa kwenye ndege hiyo ambayo ilikuwa imekodiwa na kampuni ya ulinzi ya Saracens, iliyo na makao yake nchini Uganda na afrika Kusini.