Aston Villa yajikwamua eneo baya mkiani

Aston Villa imefanikiwa kujiondoa katika eneo la kushuka daraja, baada ya kusawazisha bao na kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Birmingham. Matokeo hayo yamezipatia timu zote pointi moja.

Image caption James Collins akishangilia bao la kusawazisha la Aston Villa

Birmingham nao wamo katika patashika kubwa ya kujinasua kutoka eneo ambalo ni la hatari.

Wakicheza nyumbani, Birmingham walikuwa wa kwanza kupachika bao kipindi cha pili lililofungwa na Roger Johnson kwa mkwaju wa juu wa karibu.

Lakini Villa wakajiuliza na kushambulia kwa nguvu na kufanikiwa kusawazisha kwa balo la James Collins, aliyeunganisha mpira uliopigwa kwanza na Gabriel Agbonlahor, aliyekuwa ndani ya sanduku la hatari.

Villa walipiga mikwaju iliyogongwa mwamba wa lango la Birmingha mara nne, lakini Birmingham nao walikosa nafasi nyingi za kupata mabao, katika mchezo ambao wangeweza kushinda.