Vijana Tunis wapambana na Polisi mitaani

Vijana katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, wamepambana na polisi barabarani na kuchoma moto majengo kadhaa ya serikali, huku wakipinga amri ya serikali ya kupiga marufuku marufuku watu kutembea usiku.

Image caption Ghasia Tunisia

Maafisa wa jeshi wanashika doria katika barabara zote za mji huo, kufuatia machafuko ya mwezi mzima yaliyosababisha vifo vya waandamanaji kadha waliokabiliana na polisi.

Bunge la nchi hyo linatarajiwa kufanya kikao cha dharura kujadili mzozo huo.

Maandamano hayo yaliyosambaa kwa miji mengine nchin humo, yamesababishwa na umaskini na ukosefu wa ajira, ambao waandamanaji wanadi umesababishwa na ufisadi mkubwa serikalini.