Mancini atetea mbinu dhidi ya Arsenal

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini, ametetea mbini za timu yake, baada ya kuzomewa uwanjani kufuatia kwenda sare ya kutofunganan na Arsenal kwenye uwanja wa Emirates wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya soka ya England.

Image caption Roberto Mancini na wachezaji wake

Manchester City ilipocheza na Arsenal, iliweza kugonga milingoti ya lango mara tatu, wakati wachezaji wa timu hiyo wakionekana kutofanya jitahada za kusonga mbele, zaidi ya kukaa na mpira.

Lakini Mancini akajitetea: "Nilipenda kupata pointi angalao moja na akauliza, kipi bora kuzomewa uwanjani au kuondoka na pointi moja na kupongezwa nje ya uwanja.

"Tulitaka kushinda, lakini wakati mwingine, timu nyingine hucheza vizuri zaidi kuliko wewe na iwapo inatokea hivyo, basi jitahidi usipoteze mchezo."

City wanaendelea kushikilia nafasi ya pili ya msimamo wa ligi baada ya sare na Arsenal, pointi mbili nyuma ya wanaoongoza ligi hiyo, Manchester United wakiwa wamecheza mechi mbili zaidi ya majirani wao hao.

Katika mechi hiyo, Mancini hakuwachezesha David Silva, Mario Balotelli na Aleksandar Kolarov walio majeruhi na akasema si jambo rahisi watu kutarajia Manchester City, wanaweza kushinda kila mchezo na hasa nje ya uwanja wa nyumbani.

Manchester City katika mchezo dhidi ya Arsenal kwa dakika zote tisini hawakuweza kufyatua kombora lolote lililolrnga la wapinzani wao.