PFA wamtetea Babel na picha ya Twitter

Mkuu wa chama cha wacheza soka wa kulipwa cha England, PFA, Gordon Taylor amekielezea kwa mzaha, Chama cha Soka, FA, kama ni "watakatifu sana" kutokana na uamuzi wao wa kumshtaki mshambuliaji wa pembeni wa Liverpool, Ryan Babel, kutokana na picha na taarifa alizoandika katika ukurasa wake wa Twitter.

Image caption Ryan Babel

Babel aliihusisha picha aliyotengeneza ya mwamuzi Howard Webb, akiwa amevaa fulana ya Manchester United, baada ya Liverpool kufungwa bao 1-0 na Man United, katika mchezo wa kuwania Kombe la FA siku ya Jumapili.

"Utani wetu katika soka unaelekea wapi hivi sasa?" Aliuhoji Taylor, Mkuu wa Chama PFA.

"Aliomba radhi, wacha hayo yapite na tusonge mbele," aliongeza Taylor alipohojiwa na BBC.

Babel, ambaye ametuhumiwa kwa utovu wa nidhamu na FA, baadae aliondoa picha hiyo na akaaomba radhi katika ukurasa wake wa Twitter.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 24 maoni yake ya awali yalitokana na Liverpool kufungwa na 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya tatu wa Kombe la FA, katika uwanja wa Manchester United wa Old Trafford.

Babel ameshtakiwa haraka sana na bado mchezaji huyo aliyekiri si tu kujiangusha kwa makusudi, lakini alieleza alikuwa anamtania tu mwamuzi, jee yote hayo hayatiliwi maanani na FA?

Kwa kuongezea katika aliyoweka kwenye Twitter ya kuitengeneza picha ya Webb, Babel aliandika: "Na wanamwita mmoja ya waamuzi bora. Huo ni utani tu."

Mchezaji huyo anayechezea timu ya taifa ya Uholanzi, alipata wasomaji zaidi ya 166,000 wanaotumia Twitter kufuatia aliyoandika pamoja na picha ya Webb, ambayo baadae ikachapishwa pia katika vyombo vya habari.

Ryan Giggs alipachika bao pekee kwa mkwaju wa penalti baada ya mwamuzi Webb kudai, Daniel Agger alimkwatua Dimitar Berbatov ndani ya eneo la sanduku la hatari, dakika ya kwanza tu ya mchezo.

Webb baadae alimto nje kwa kadi nyekundu Steven Gerrard, katika dakika ya 32 kutokana na kumchezea rafu mbaya Michael Carrick.

Meneja wa Liverpool, Kenny Dalglish, aliita penalti hiyo kama ni "mzaha"na pia hakukubaliana na kadi nyekundu aliyooneshwa nahodha wake.