Uwanja wa Olympic watetewa usibadiliswhe

Meneja wa wanariadha wa Uingereza Ed Warner, amesema kuondoa sehemu ya riadha kwenye uwanja wa Olimpiki wa London mwaka 2012 ni kukiuka mkataba.

Image caption Uwanja mpya wa Olympic London

Klabu za ligi ya Ligi Kuu za England, Tottenham na West Ham wanawania haki za kuimiliki uwanja huo na Tottenham imesema wataondoa sehemu ya riadha katika uwanja huo.

'Ni kukiuka mkataba,' alisema Warner.

'Ahadi zilitolewa na jumuiya ya wanamichezo inatazamia Uingereza itatimiza ahadi zake.'

Aliongezea: 'Pindi unapoinvunja imani kwa kiwango hicho, huwezi kuaminika tena katika mchakato wa kuandaa michuano.

Baadhi ya wanachama wa IOC ambao wameeleza bayana baadhi ya sababu za kuichagua London, ni kwa sababu London inahitaji shime ya uwanaridha ambayo haipo.

Warner amesisitiza bila uwanja wa wanariadha, itakuwa vigumu sana kwa London London kuwavutia wanariadha.

'Uingereza haina jina nzuri na Shirikisho la Riadha la kimataifa- IAAF katika kuandaa mashindano makubwa ya ubingwa wa dunia ya riadha.

Tungependa kuandaa mashindano ya mbio za ubingwa wa dunia mwaka 2017 au mashindano yatakayofuata na ni lazima tuwe na miundombinu.

Warner amesema alistaajabishwa na mvuto wa soka katika jambo hili.