Rais mstaafu Obasanjo azuru Ivory Coast

Rais mstaafu wa nigeria, Olusegun Obasanjai yuko nchini Ivory Coast ili kumshinikiza Rais Gbagbo aache urais.

Image caption Rais mstaafu wa Nigeria, Bw Obasanjo

Msemaji wa Alassane Ouattara - ambaye anatambuliwa na wengi kama mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi wa November - amesema Bw. Obasanjo amefanya mazungumzo na Bw Ouattara na Bw Gbagbo katika vipindi tofauti.

Hakuna maelezo zaidi kuhusu mazungumzo hayo lakini msemaji wa Bw Ouatarra amesema kuwam azungumzo zaidi zitafanyika leo Jumapili.

Jumuiya ya Afrika Magharibi, ECOWAS, imetishia kumng'oa Bw. Gbagbo madarakani kwa nguvu iwapo ataendelea kung'ang'ania madaraka.