Kiongozi wa Nigeria apata changamoto

Bw Atiku Abubakar
Image caption Bw Atiku Abubakar

Chama tawala Nigeria kinatarajiwa kuchagua mgombea wake katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi Aprili.

Changamoto kubwa anayotarajiwa kukabiliana nayo Rais Goodluck Jonathan ni kutoka kwa aliyekuwa makamu wa Rais Atiku Abubakar.

Mgombea wa PDP ameshinda kila uchaguzi tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999, kwahiyo mgombea wake anatarajiwa kuungwa mkono zaidi.

Lakini baadhi ya wachambuzi wanasema PDP kinaweza kugawanyika kutokana na kura za watu wa kusini zinazomwuunga mkono Bw Jonathan na Bw Abubakar anayeungwa mkono na upande wa kaskazini.

PDP kina desturi ya kubadilishana uongozi baina ya kaskazini na kusini baada ya kukaa madarakani kwa mihula miwili lakini hii ilivurugwa baada ya Bw Jonathan, kutoka kusini, kumrithi Umaru Yar'Adua alipofariki mwaka jana.

Kuna ulinzi wa hali ya juu katika mji mkuu, Abuja, ambapo upigaji wa kura hizo unapofanyika, kufuatia mashambulio ya mabomu ya hivi karibuni.