Huwezi kusikiliza tena

Tanzania yabanwa isilipe deni

Wananchi na taasisi mbali mbali nchini Tanzania wamezidi kupinga hatua ya serikali kuelezea kukubali kulipa fidia ya dola milioni 65 kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans Holdings SA, baada ya mahakama ya kimataifa ya mashauri ya biashara kuamua kuwashirika la kusambaza umeme la taifa, TANESCO, lilikatisha mkataba kinyume cha sheria.

Huku waziri mmoja wa serikali akipinga wazi wazi mpango wa serikali kukubali kulipa fidia hiyo, leo kituo cha sheria na haki za binadamu nchini humo, LHRC, kimefungua shauri katika mahakama kuu ya Tanzania kupinga Dowans Holdings SA kulipwa. Mwandishi wetu Josephat Mwanzi anasimulia kutoka Dar Es Salaam.