Upigaji kura Sudan yamalizika

Shughuli ya upigaji kura imekamilika baada ya wiki moja katika kura ya maoni itakayoamua iwapo Sudan Kusini itajitenga au la.

Image caption Wapigaji kura wakipiga foleni

Katika taarifa iliotangazwa moja kwa moja kwenye runinga, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Professor Ibrahim Khalil alisema shughuli hiyo ilikwenda vizuri huku asilimia sitini ya waliojiandikisha wakipiga kura.

Kura hiyo ilikuwa mojawapo wa makubaliano yalioafikiwa katika juhudi za kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya zaidi ya miongo mitano nchini Sudan.

Matokeo ya mwanzo ya kura hiyo yanatarajiwa mwishoni mwa mwezi huu.