Martin O'Neil akataa umeneja West Ham

West Ham "imepania kumbakisha Avram Grant kuendelea kuwa meneja wao" baada ya taarifa zilizomhusisha Martin O'Neill kuchukua kazi yake.

Image caption Avram Grant

Kitengo cha michzo cha BBC, kimepata taarifa kwamba O'Neill, aliyeondoka Aston Villa mwezi wa Agosti, aliamua mwishoni mwa wiki kutochukua nafasi ya Grant.

West Ham wapo mkiani katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, lakini ilishinda mechi zake tatu kati ya sita zilizopita chini ya usimamizi wa Grant.

Lakini taarifa ya klabu hiyo imesema "walengwa wakati huu wa usajili wameshamulikwa", ili kuiokoa klabu hiyo isiteremke daraja."

Mlinzi wa kushoto wa Manchester City, Wayne Bridge, aliyesajiliwa kwa mkopo na hadi mwishoni mwa msimu huu, ndiye pekee aliyetua katika klabu hiyo wakati huu wa dirisha dogo la usajili.

Taarifa za awali zilidai kwamba O'Neill alikuwa karibu kuchukua hatamu za uongozi wa timu hiyo baada ya mchezo dhidi ya Arsenal siku ya Jumamosi.

West Ham haikutoa taarifa yoyote kuhusiana na suala la nafasi ya meneja mara baada ya kufungwa na Arsenal mabao 3-0, ingawa sasa imejieleza kuhusiana na nafasi ya Grant.