Wenyeji Sudan yasema Chan itafanikiwa

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Sudan, ametoa uhakikisho wa kufanikiwa mashindano ya Ubingwa wa Afrika maarufu Chan.

Image caption Caf

Sudan watakuwa wenyeji wa mashindano hayo mwezi wa Februari, ambapo timu zitaongezeka safari hii kutoka nane hadi 16.

Na licha ya matatizo yaliyokumba maandalizi yake, Dokta Hassan Abou Jabal, amesema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi.

Aliiambia BBC mjini Khartoum: "Tuna hakika kila kitu kitakuwa sawa."

Sudan inandaa mashindano hayo ya pili, yanayohusisha wachezaji wanaochezea ligi za nyumbani, kuanzia tarehe 4 hadi 25 mwezi wa Februari.

Kumekuwa na lawama kwa maandalizi kuchelewa, lakini Dokta Abou Jabal, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Sudan, amesema kila kitu kitakamilika kwa ajili ya mashindano hayo.

Amesema: Tumehakikishiwa viwanja sehemu ya kuchezea, vitakuwa tayari kabla ya mwisho wa mwezi wa Januari."