RaisYemen asema hatagombea baada ya 2013

Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen amesema hatagombea Urais wakati muhula wake utakapomalizika mnamo mwaka 2013, kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais Ali Abdullah Saleh

Bwana Saleh, ambaye amekuwa madarakani kwa miongo mitatu, pia aliahidi hatamkabidhi madaraka mwanawe..

Aliliambia bunge kabla ya maandamano yaliyopangwa katika mji mkuu Sanaa siku ya Alhamisi na ikiigiza maandamano ya Tunisia na Misri,y emepewa jina " siku ya ghadhabu".

Bwana Saleh alishika madaraka ya Urais wa Yemen ya kaskazini mwaka 1978.

Nchi hiyo ilipoungana na Yemen ya Kusini mwaka 1990 alishika wadhifa wa Rais wa Jamhuri mpya. .

Akihutubia kikao cha dharura cha Bunge la nchi hiyo na Baraza la ushauri, alielezea mipango yake ya kuondoka madarakani.

"Hakuna kuongeza muda, hakuna kurithi madaraka, wala kurudisha saa nyuma ," alisema Bw. Saleh.

"Ninatoa mapendekezo haya kwa maslahi ya nchi. Maslahi ya nchi yanapaswa kuzingatiwa dhidi ya maslahi yetu binafsi.,," alisema

Pia aliutaka upande wa upinzani usimamishe maandamano na mikutano yote yaliyopangwa.