Mkusanyiko wa "siku ya kuondoka" Misri

Umati mkubwa umekusanyika kwenye eneo la wazi katik mji mkuu wa Misri, Cairo, kushinikiza madai ya kujiuzulu kwa rais Hosni Mubarak.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Maelfu wamekusanyika Cairo

Maelfu ya waandamanaji waliohudhuria "siku ya kuondoka" katika mkusanyiko huo kwenye eneop la Tahrir wamepeperusha bendera huku wakiimba "ondoka! Ondoka!".

Wanajeshi wamekuwa wakilinda eneo hilo ili kuzuia mfarakano kati yao na wanaomuunga mkono rais Mubarak.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanaji Cairo

Bw Mubarak amesema "amechoshwa" kukaa madarakani, lakini hataki kujiuzulu kwa sababu hatua hiyo italeta machafuko.

Amekiambia kituo cha televsheni cha ABC News kuwa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood, litachukua nafasi ya utawala iwapo ataondoka.

Pia amekanusha kuwa utawala wake ulihusika na ghasia zilizotokea siku mbili zilizopita, na taarifa kuwa mwanaye, Gamal, ana nia ya kuwania urais.