Chagizo la kiuchumi litamuondoa Gbagbo

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast, Young-Jin Choi, amesema chagizo za kiuchumi huenda zikamlazimisha kiongozi wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, kuondoka madarakani baada ya maelfu ya wanajeshi na wafanyakazi wa serikali kukosa mishahara mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Laurent Gbagbo

Akizungumza baada ya mkutano wa faragha wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Bw Choi alisema matatizo ya kiuchumi yanaweza kumaliza mzozo juu ya hatu za kumkabidhi madaraka mtu anayesadikika kwa kiasi kikubwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa mwaka jana, Alassane Ouattara.

Bw Choi alisema itakuwa vigumu kwa Bw Gbagbo kuendelea kutawala baada ya benki ya kikanda ya mataifa ya Afrika Magharibi kusitisha ufadhili wake kwa nchi hiyo.