Uganda yatoa hadhari ya kufanyika ugaidi

Polisi nchini Uganda wametoa hadhari mpya dhidi ya kutokea tukio la kigaidi. Hadhari hii imetolewa wakati huu wakati ucahguzi mkuu ukiwa unakaribia.

Image caption Polisi wa Uganda

Mkuu wa polisi nchini Uganda Meja Jemedari Kale Kaihura ametoa onyo la kutokea shambulio la kigaidi na hivyo kuwapa hadhari wananchi.

Maelezo zaidi ni kuwa tisho la shambulio la kigaidi linatokana na kundi la Al Shabaab na linapangwa siku za mwisho za kampeni pamoja na uchaguzi.

Kampeini za Urais na Ubunge zinaendelea na zimepangwa kumalizika tarehe 16 mwezi huu wa Februari na uchaguzi utafanyika tarehe 18 mwezi huu wa Februari.

Polisi wametoa hadhari kwa wananchi kuwa waangalifu na kuripoti watu wasioeleweka kwa vyombo vya usalama, pamoja na vifurushi ambavyo wanashuku vikiwa vimeachwa mahali.