Chelsea yachemsha kwa Liverpool

Chelsea imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na pia wachezaji wake wapya iliyowasajili, kwa kufungwa bao 1-0 na Liverpool.

Haki miliki ya picha 1
Image caption Raul Meireles

Fernando Torres wa Chelsea ambaye ndiye alikuwa gumzo kabla ya kuanza kwa mchezo, hakuweza kuwika na kupata goli dhidi ya timu yake ya zamani.

Timu zote zililikuwa zikicheza mchezo wa kutegeana kwa karibu muda wote.

Bao pekee na la ushindi lilipatikana katika dakika ya 69 baada ya krosi ya Steven Gerrard kumkuta Raul Meireles aliyepachika bao hilo.

Chelsea inaendelea kusalia katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 44, sawa na Tottenham, huku Liverpool ikijikita katika nafasi ya sita ikiwa na pointi 38.