Licha kufungwa Ferguson asifu timu yake

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson, ameipongeza timu yake licha ya rekodi yake ya kutopoteza mechi 29 ilipofika ukingoni baada ya kulazwa 2-1 na Wolves.

Image caption Sir Alex Ferguson

Vinara hao wa Ligi Kuu ya England, kupoteza mchezo wao wa kwanza msimu huu wa ligi, kumewapa matumaini wapinzani wake, lakini Ferguson kukataa kuwashutumu wachezaji wake.

"Wachezaji wetu wametufanya tutembee kifua mbele," alisema Ferguson, huku akikiri kuhuzunishwa na matokeo hayo.

"Ilikuwa ni nafasi yetu ya kuendelea kufanya vizuri kama tulivyokuwa mwanzoni, lakini kutetereka kulikojitokeza miezi miwili iliyopita hakukupendeza."

Manchester United waliocheza chini ya kiwango chao cha kawaida walikuwa wa kwanza kuongoza kwa bao la mapema lililofungwa na Nani, lakini huo ulikuwa ndio wasaa wao pekee mzuri baada ya George Elokobi na Kevin Doyle kuipatia Wolves wanaoshikilia mkia ushindi muhimu.

Ferguson alisema:"Nilisema kabla ya mechi, sidhani Wolves kama wapo nafasi mbaya.

Msaidizi wa Ferguson, Mike Phelan, alikataa kulaumu kukosekana kwa Rio Ferdinand dakika za mwisho, aliyeumia goti wakati wa mazoezi ya kupasha moto na sasa hatacheza kwa wiki mbili.