Ndege yakamatwa na dhahabu, Congo

Serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imesema kuwa imeikamata ndege ikiwa imebeba kilo 435 za dhahabu na zaidi ya dola za kimarekani milioni sita kwenye ndege hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dola za Marekani

Gavana wa Kivu Kaskazini, Julien Paluku, amesema Wanigeria watatu, Wamarekani wanne na Mfaransa mmoja wamekamatwa.

Ripoti zinasema kuwa dhahabu na pesa hizo , baadhi yake zikwa ni za bandia, zinadhaniwa kutoka kwa aliyekuwa Kamanda wa waasi, Jenerali Bosco Ntaganda, ambaye anasakwa na mahakama ya kimataifa kwa uhalifu wa kivita.

Gavana wa mkoa wa Kivu ya kaskazini anahisi vitendo hivyo ni vya kuchochea vita na biashara ya madini ni marufuku mashariki mwa Congo.