Huwezi kusikiliza tena

Kiwango cha elimu chashuka Tanzania

Mjadala kuhusu kiwango cha elimu nchini Tanzania kinachoelezwa kushuka, bado unazidi kuendelea nchini humo.

Mjadala huo umezidi kuwa mzito baada ya matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2010 yaliyotolewa hivi karibuni kuonyesha karibu nusu ya wanafunzi walifanya vibaya katika masomo.

Kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa wadau wa elimu na wananchi wa kawaida, wakidai huenda moja ya sababu iliyoshusha kiwango hicho ni mfumo mzima wa elimu ambao haulingani na mazingira halisi ya nchi hiyo kwa sasa.

Kutoka Dar es Salaam mwandishi wetu John Solombi ametutumia taarifa ifuatayo.