Mechi za Ubingwa wa Afrika zaahirishwa

Mechi kadha za Ubingwa wa vilabu barani Afrika zimeaahirishwa kutokana na kuendelea kwa mashindano ya Chan .

Shirikisho la Soka barani Afrika, Caf, imeahirisha mechi kadha za kutafuta klabu bingwa zilizopangwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii.

Mechi zitakazoathirika ni za vilabu vyenye wachezaji takriban watatu wanaoshiriki mashindano ya kutafuta bingwa wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani, yanayoendelea nchini Sudan.

Katika mechi zote tisa za Ubingwa wa vilabu, sasa zitachezwa katika tarehe itakayopangwa baadae, wakati mechi nyingine sita za kuwania Kombe la Shirikisho pia nazo zimeathiriwa na mashindano ya Chan.

Taarifa iliyotolewa na Caf imesema mechi hizo sasa zitachezwa wiki ya mwisho ya mwezi wa Februari.

Mechi zifuatazo zimeahirishwa:

Ubingwa wa Vilabu Afrika

JC Abidjan (CIV) v ASFAN (NIG)

Astres Douala (CMR) v US Bitam (GAB)

Djoliba (MLI) v East End Lions (SLE)

Cansado (MTN) v ASEC Mimosas (CIV)

Club Africain (TUN) v. APR (RWA)

Aduana Stars (GHA) v Wydad Casablanca (MAR)

Cotonsport Garoua (CMR) v Vital'O (BDI)

Vita Club (COD) v Ocean View (ZAN)

Zamalek (EGY) v Ulinzi Stars (KEN)

Kombe la Shirikisho Afrika:

AS Real (MLI) v Tevragh Zeina (MTN)

Sahel (NIG) v Dynamic (TOG)

AshantiGold (GHA) v Sewe San Pedro (CIV)

Africa Sport (CIV) v Sequence (GUI)

Inter Stars (BDI) v Missile (GAB)

DC Motema Pembe (COD) v KMKM (ZAN)