Maandamano Misri yawa madai ya mishahara

Maandamano mapya na migomo imeikumba Misri, kufuatia wafanyakazi kudai mishahara mizuri zaidi na mazingira bora ya kazi kutoka kwa watawala wapya wa kijeshi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wafanyakazi wakifanya mgomo Cairo

Wafanyakazi wa benki, usafiri wa umma na utalii waliandamana mjini Cairo, siku 18 baada ya maandamano yaliyofanikiwa kumuondoa Rais Hosni Mubarak.

Katika taarifa kupitia televisheni, jeshi limewataka wafanyakazi wote kurejea kazini.

Mapema, eneo la wazi la Tahrir, waandamanaji waliondolewa, lakini muda mfupi baadaye mamia walirejea, akiungwa mkono na polisi waliokuwa wakinung'unika.

Mamia ya polisi wenye sare na wengine wasio kuwa nazo, waliandamana kuelekea Tahrir, huku wakipiga kele: "Sisi na raia ni sawa" na kuahidi "kuenzi mashujaa wa mapinduzi".

Wamesema wamelazimishwa kufanya matendo kinyume na matakwa yao, katika kutumia mguvu dhidi ya waandamanaji, mapema wakati maandamano yakianza.